TETESI ZA SOKA: Liverpool yaanza mazungumzo na Amorim
Eric Buyanza
April 5, 2024
Share :
Imeripotiwa kuwa klabu ya Liverpool tayari imeshaanza mazungumzo na mkufunzi wa Sporting Lisbon Ruben Amorim, ili kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp.
Hata hivyo kumekuwa na mjadala kuhusu gharama za kumchukua Amorim ambapo inakadiriwa gharama za kuvunja mkataba wake pale Lisbon ni takriban pauni milioni 8.5.