TETESI ZA SOKA: Man U, Liverpool waungana na Arsenal kufukizia saini ya Hato
Eric Buyanza
March 18, 2024
Share :
Soka Liverpool na Manchester United wameripotiwa kuungana na Arsenal katika mbio za kumsajili beki mchanga wa Ajax, Jorrel Hato.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 hivi majuzi ameisaini kandarasi mpya na wababe hao wa Amsterdam hadi mwaka 2028 ambao umemfanya kuwa nahodha mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya Ajax.