TETESI ZA SOKA: Man United mbioni kumsajili beki wa Bayern Munich
Eric Buyanza
July 10, 2024
Share :
Manchester United wako mbioni kumshusha Old Trafford beki wa Bayern Munich Mholanzi, Matthijs De Ligt.
Duru zinasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka miaka 24 tayari ameshafanya makubaliano binafsi ya awali na Manchster United.
United wako tayari kumpa De Ligt, mkataba wa miaka mitano ikiwa mambo yataenda kama inavyotarajiwa.