TETESI ZA SOKA: PSG waandaa dau la pauni milioni 80 kumnunua Rashford
Eric Buyanza
March 14, 2024
Share :
Gazeti la Daily Mirror linaripoti kuwa Paris St-Germain wameandaa dau la pauni milioni 80 kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, na watakuwa tayari kumlipa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 takriban pauni 500,000 kwa wiki.
Paris St-Germain wanahitaji saini ya Rashford ili kumrithi Kylian Mbappe.
#TetesiZaSoka