Tetesi zilisema Berkane wamepindua meza usiku wa leo ametua Chile.
Joyce Shedrack
August 3, 2026
Share :
Mchezaji wa Kombe la Dunia wa Cape Verde, Vozinha ametua Santiago kukamilisha uhamisho wake kwenda kwa vigogo wa Chile, Colo-Colo, baada ya wiki kadhaa za ucheleweshaji wa kiutawala.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 40 alipokelewa kwa shangwe kubwa uwanjani, ambapo mamia ya mashabiki wenye furaha walikusanyika kumkaribisha na kusherehekea usajili wake mkubwa wa katikati ya msimu.
Colo-Colo ilitangaza rasmi usajili wa kipa mwenye umri wa miaka 40, Josimar Evora Dias, anayejulikana zaidi kama Vozinha, mnamo Julai 24 akitokea klabu ya daraja la pili nchini Ureno, Chaves.
Hata hivyo, matatizo ya nyaraka pamoja na masuala binafsi yalichelewesha safari yake mara tatu tofauti, jambo lililosababisha wasiwasi kwa uongozi wa klabu huku RS Berkane ikitajwa kuwa kwenye mipango ya kupindua meza.





