pmbet

TFF Yaufungulia uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Joyce Shedrack

May 15, 2026
Share :

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungulia uwanja wa Jamhuri, Dodoma kutumika kwa michezo ya Ligi baada ya kufanya marekebisho yaliyokidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
No photo description available.
Uwanja huo uliofungiwa kutokana na miundombinu yake kutofaa kutumika kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu umekaguliwa na kukidhi vigezo vya Kikanuni baada ya marekebisho yaliyoelekezwa kufanyika.

Hata hivyo TFF inaendelea kuzikumbusha klabu kuendelea kuboresha na kutunza miundombinu ya viwanja vyao vya nyumbani kwa kushirikiana na wamiliki kwa klabu ambazo hazimiliki viwanja, ili michezo ya Ligi ichezwe kwenye viwanja bora vinavyosaidia kuongeza ushindani na thamani ya Ligi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet