pmbet

Thabo Bester aomba kuhukumiwa kifo mahakamani, Jaji apagawa

Sisti Herman

June 6, 2024
Share :

Mtuhumiwa wa mauaji na ubakaji, Thabo Bester, jana aliiomba Mahakama Kuu ya Free State nchini Afrika kusini, kutoa hukumu ya kifo dhidi yake na kuwaachilia washtakiwa wenzake.

Akihutubia, Bester ambaye alijiwakilisha mwenyewe baada ya mawakili wake kujitoa kwenye kesi hiyo, kwa madai ya kutolipwa ada.

"Ninahisi sio haki kwa watu hawa ambao wameketi hapa kuitwa washtakiwa wenzangu kuwa mahakamani wakati najua vizuri kwamba hawana uhusiano wowote na hili.

"Mheshimiwa, nasema haya kama mtu aliyevunjika na nasema haya kwa moyo wote, inanitia machozi kuwaona watu hawa katika mahakama hii, najua kwamba wanateseka kwa kitu ambacho hawajui," alisema.

Akinukuu sheria ambayo imefutwa tangu kushtakiwa, aliomba apewe adhabu ya kifo kupitia ombi ambalo litatiwa saini na umma.

Thabo Bester, Nandipha Magudumana (Mpenzi wake) na washtakiwa wenzake wamerejea mahakamani mwaka mmoja tangu Thabo Bester na Dk Nandipha Magudumana warudishwe nchini humo baada ya kukamatwa jijini Arusha Tanzania wakiwa wametoroka gerezani nchini Afrika kusini.

“Mara moja nitakubaliana nayo na tunaweza kumaliza jambo hili. Nilikuja hapa na magari 80, niliamka saa 2 asubuhi. Nimekuwa na minyororo kwenye miguu yangu. Miguu yangu ni barafu. Siwezi kuhisi vidole vyangu kwa wakati huu. Hii sio njia ninayotaka kuendelea, mheshimiwa.

"Ikiwa na maana kwamba mahakama hii inaweza kukubali ombi hilo na umma unaweza kusaini, basi tunaweza kuhitimisha sakata hili. Nina amani. Ninajua nilichofanya na ambacho sijafanya,” Bester aliambia mahakama.

Bester alisema kuwa "hakuna lolote kati ya haya" lingetokea ikiwa "hakukuwa na shinikizo lolote la kisiasa".

Bester aliyejawa na hisia kali aliishambulia Magereza, akidai kwamba hata alipokuwa akishauriana na wanasheria wake, simu zao zilikuwa zikirekodiwa na anahofia hali yake ya kiakili, kwani hakuwahi kuwasiliana na watu, isipokuwa mlinzi alisimama nje ya seli yake, katika muda wa miezi 15. Alizidi kushutumu vyombo vya habari kwa jinsi alivyokuwa akionyeshwa na makala zilizoandikwa kumhusu.

Bester pamoja na washtakiwa wenzake wanatuhumiwa kushiriki tukio la 'mwamba' huyo kutoroka gereza la Mangaung, watarejea mahakamani Julai 25.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet