pmbet

Thabo Senong' ataja kwanini ligi ya Tanzania ni bora, aiweka Kariakoo Derby 'Top 5' Africa

Sisti Herman

May 23, 2024
Share :

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Singida Fountain Gate FC na timu ya Taifa ya vijana ya Afrika kusini Thabo Senong' akiwa kwenye mahojiano maalumu na Kipindi cha michezo cha Arena Sports Show kinachorushwa na televisheni ya Times ya Afrika kusini ametaja sifa nzuri za ligi kuu Tanzania bara ambazo zimeifanya kuwa moja kati ya ligi zinazovutia barani Afrika.

 

"Ni ligi ngumu yenye ushindani kwasababu;

 

1. kwasababu mpira wa miguu ndiyo mchezo unaotazamwa sana haishindani na michezo kama ilivyo hapa (Afrika kusini)"

 

2. Sheria ya wachezaji wa kigeni inaruhusu na kutoa fursa kwa wageni wengi wenye uwezo mkubwa kujiunga na timu zao mfano imekusanya vipaji kutoka maeneo tofauti, ndani na nje ya Afrika, kuna vipaji kutoka Afrika Magharibi, kaskazini na kusini na hata nchi za jirani na pale huitazama kama kioo"

 

3. Wana makocha kama Benchikha kutoka Afrika kaskazini, Gamondi kutoka Amerika kusini pia aliwahi kufundisha Mamelodi Sundowns nafuraha sana kuwa mmoja wa walifundisha ile ligi na nimejifunza mengi"

 

Najua kuna namna itaathiri timu yao ya Taifa lakini kwa ushindani utakaokuwepo hata timu yao ya Taifa itaimarika.

 

Alipoulizwa kuhusu hamasa ya dabi ya kariakoo kati ya Simba na Yanga Thabo aliendelea;

 

"Kuna dabi ya Simba na Yanga, moja kati ya Dabi bora zaidi kwasasa kwenye bara hili, ipo kwenye tano bora, mashabiki wa hizo timu wanahamasa Sana na timu zao, wanashinikiza ushindi kwa wachezaji wao, ukifanya vyema mashabiki wanakupenda"

 

"Ni dabi yanye wachezaji wa viwango vya juu sana, wachezaji wanaotoka timu za Taifa, kwao na mataifa mengine"

 

Hiyo ilikuwa sehemu ya mahojiano hayo ya Thabo Senong'

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet