Thabo Senong' awa Mkufunzi wa Makocha CAF leseni 'B' Sauzi
Sisti Herman
May 7, 2024
Share :
Aliyekuwa kocha wa Singida Fountain Gate FC Thabo Senong' amepewa majukumu ya kuwanoa makocha wanaosoma kozi za Ukocha kutafuta leseni B ya CAF.
Shirikisho la soka nchini Afrika Kusini "SAFA" limempa majukumu hayo Thabo Senong ambaye pia ni Mkufunzi wa CAF kuwanoa makocha hao ambao wengi ni wachezaji wa zamani wa nchi hiyo.
Senong aliachana na Singida baada ya klabu hiyo kupitia misukosuko mbalimbali ya kiutawala na kiuchumi yaliyosababisha kubadili makocha hadi kufikia wanne huku ikiondokewa na wachezaji kila kukicha.