pmbet

Thomas Muller na rekodi ya kipekee ligi ya mabingwa Ulaya

Joyce Shedrack

March 6, 2024
Share :

Mchezaji wa timu ya Taifa Ujerumani na  klabu ya Bayern Munich  Thomas Muller amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka Nchini  Ujerumani kuweka rekodi kufunga magoli mengi zaidi kwenye mashindano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

 

Muller ambaye ana umri wa miaka 34, mpaka sasa ametupia kambani magoli 54 katika michezo 149 aliyocheza kwenye mashindano hayo makubwa zaidi kwa ngazi ya klabu barani Ulaya.

 

Mshambuliaji huyo wa The Bavarians amefikisha idadi ya magoli 54 wakati akifunga goli  siku ya jana klabu yake ilipokutana na Lazio na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0 ushindi ulioipeleka Bayern Robo Fainali ya mashindano hayo.

 

Goli hilo limemfanya Muller kuendelea kushika nafasi ya nane katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa michuano hiyo nyuma ya Andriy Shevchenko mwenye magoli 59,orodha hiyo inaongozwa na Cristiano Ronaldo aliyefunga magoli 141, Lionel Messi magoli 129, nafasi ya 3 yupo Robert Lewandowski 93, Karim Benzema,90, Raul,71, na namba sita akiwa ni Ruud van Nisterlooy aliyetupia kambani magoli 60.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet