pmbet

Thomas Partey akabiliwa na mashtaka ya ubakaji

Eric Buyanza

February 13, 2026
Share :

Mchezaji wa zamani wa Arsenal Thomas Partey ameshtakiwa kwa makosa mawili ya ubakaji dhidi ya anayedaiwa kuwa mwathiriwa mpya.

 

Hatua hiyo inakuja baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 hapo awali kukana mashtaka matano ya ubakaji dhidi ya wanawake wawili, na shtaka moja la unyanyasaji wa kingono linalodaiwa kuhusishwa na mwanamke wa tatu.
 

Ina maana Partey sasa anatuhumiwa kwa makosa ya kingono dhidi ya wanawake wanne.
 

Mashtaka hayo mawili mapya yanahusiana na makosa yanayodaiwa mwaka 2020 ambayo yaliripotiwa kwa mara ya kwanza kwa polisi Agosti mwaka jana.

Madai hayo yanafuatia uchunguzi mpya kutoka kwa Polisi wa Metropolitan.

Partey atafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Westminster tarehe 13 Machi kwa ajili ya kusikilizwa kwa mara ya kwanza kuhusiana na mashtaka mawili mapya.

 

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana alipewa dhamana ya masharti katika Mahakama ya Southwark Crown mwezi Septemba baada ya kujibu bila hatia mashitaka matano ya awali.
 

Makosa hayo ambayo alishtakiwa nayo mwaka jana, yalifanyika kati ya 2021 na 2022 alipokuwa akiichezea klabu ya Arsenal ya London kaskazini.
 

Alishtakiwa siku nne baada ya kuondoka Arsenal wakati mkataba wake ulipomalizika mwishoni mwa Juni.

 

Mashtaka hayo yalifuatia uchunguzi wa wapelelezi, ambao ulianza Februari 2022 baada ya polisi kupokea ripoti ya ubakaji kwa mara ya kwanza. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa chini ya jaji wa Mahakama Kuu tarehe 2 Novemba mwaka huu.


 

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet