Tijjani Reijnders asaini miaka 5 kuichezea Man City
Eric Buyanza
June 11, 2025
Share :
Manchester City wamekamilisha usajili wa kiungo wa AC Milan Tijjani Reijnders kwa dau la pauni milioni 46.3.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amesaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo.
Reijnders ni mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi ambaye alikuwa na mabao na asisti nyingi zaidi ya kiungo yeyote katika Ligi ya Serie A msimu uliopita.