pmbet

Tikiti maji lina nguvu sawa na Viagra - Utafiti

Eric Buyanza

July 2, 2026
Share :

Tikiti maji ni zuri kwa miili yetu, lina faida nyingi za kiafya, lakini watafiti nchini Marekani wamelinganisha tikiti maji na Viagra, dawa inayotumika kutibu tatizo la ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume

 

Viagra, ambayo pia inajulikana kama 'sildenafil', awali ilikusudiwa kusaidia moyo kwa sababu kazi yake kuu ni kuboresha mtiririko wa damu kwa kupanua mishipa ya damu.

Viagra husaidia mishipa ya damu mwilini kwa njia ile ile ambayo kemikali asilia ya citrulline inayopatikana kwenye tikiti maji husaidia mishipa ya damu mwilini.
 

'Sitrulline' iliyomo kwenye tikiti maji hulegeza mishipa ya damu mwilini ili kuboresha mzunguko wa damu. Mzunguko mzuri wa damu ndio ambao hufanya uume kusimama vizuri, damu ya kutosha inapofika katika mishipa.

 

Utafiti huu ulifanywa na Kituo cha Maendeleo ya Mboga cha Texas nchini Marekani.

Dkt. Bhimu Patel, aliyeongoza utafiti kuhusu tikiti maji, anasema, “Tunajua kwamba tikiti maji ni zuri kwa mwili. Uchunguzi bado unaendelea kuhusu faida zake zingine. Mambo mengi mazuri yanajitokeza kutokana na matumizi ya tikiti maji.”
 

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet