TikTok yarejeshwa Marekani baada ya Trump kuingilia kati.
Joyce Shedrack
January 20, 2025
Share :
Mtandao wa TikTok umerejesha tena huduma zake watumiaji wake wa Nchi ya Marekani baada ya Rais mteule anayeapishwa leo Donald Trump kusema atatoa amri ya kiutendaji ya kusitisha kuondolewa kwa mtandao huo wakati atakapoingia madarakani mara tu baada ya kuapishwa.
Siku ya Jumamosi mtandao huo unaomilikiwa na China ulisitisha kufanya kazi kwa watumiaji wa Marekani baada ya sheria inayopiga marufuku kwa misingi ya usalama wa taifa kuanza kutumika.
Siku ya Jumapili Trump ambaye awali alikuwa ameunga mkono marufuku ya jukwaa hilo aliahidi kuchelewesha utekelezaji wa sheria na kuruhusu muda zaidi wa makubaliano kufanywa.
Kupitia taarifa ya kampuni hiyo ilimshukuru Rais Trump kwa kutoa ufafanuzi na uhakikisho muhimu na kusema itafanya kazi na Trump kwa suluhisho la muda mrefu ambalo litaiweka TikTok nchini Merikani.