pmbet

Tim Cook astaafu rasmi kuwa C.E.O wa Apple baada ya miaka 15

Sisti Herman

September 1, 2026
Share :

 

Ikiwa ni baada ya muongo mmoja na nusu wa uongozi uliotukuka, Tim Cook rasmi amehitimisha safari yake ya miaka 15 akiwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kmapuni kubwa ya teknolojia duniani, kampuni ya Apple.

 

Cook, ambaye alichukua mikoba ya uongozi mwaka 2011 kutoka kwa mwanzilishi mwenza wa kampuni hiyo, marehemu Steve Jobs, anaondoka huku akiacha alama isiyofutika katika sekta ya biashara na teknolojia ulimwenguni.

 

Katika kipindi chake cha uongozi, Cook ameiwezesha Apple kushuhudia ukuaji wa ajabu wa kiuchumi. Wakati anachukua kijiti cha uongozi, thamani ya Apple sokoni ilikuwa takriban dola bilioni 350 za Marekani. Hata hivyo, kupitia mbinu zake thabiti za usimamizi wa ugavi (supply chain), kupanua soko la bidhaa, na kuanzisha huduma mpya za kidijitali, ameiwezesha kampuni hiyo kuvunja rekodi na kufikia thamani ya dola trilioni 4.

 

Ukuaji huu mkubwa umeifanya Apple kuwa moja ya kampuni zenye thamani kubwa zaidi katika historia ya mwanadamu. Uamuzi wa Cook kuhitimisha ngwe yake unatarajiwa kufungua ukurasa mpya kwa jitu hilo la Silicon Valley, huku wawekezaji na wafuatiliaji wa sekta ya teknolojia wakisubiri kwa hamu kuona mwelekeo mpya utakaochukuliwa na uongozi utakaofuata.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet