pmbet

Tim Sherwood ataka Erik Ten Hag atimuliwe!

Eric Buyanza

December 27, 2023
Share :

Meneja wa zamani wa Tottenham Hotspur, Tim Sherwood ametaja wachezaji wawili ambao Manchester United walipaswa kuwasajili katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi lililopita.
 

Sherwood pia anataka Man United wamtimue meneja wao Erik Ten Hag kwa sababu hapati matokeo mazuri kutoka kwa wachezaji wake.
 

Man Utd  wamekuwa na kipindi kigumu msimu huu, baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa na wamepoteza mechi nane kati ya 19 za Premier League.
 

Ten Hag amekabiliwa na ukosoaji kuhusu masuala kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuajiriwa kwake na mpasuko kwa wachezaji.

"Ningesema misimu miwili iliyopita kwamba Tottenham walihitaji kuchunguzwa wazi, lakini sasa wana meneja ambaye anapata matokeo bora kutoka kwa wachezaji binafsi," Sherwood aliiambia Sky Sports.
 

"Kilichofanywa na Tottenham ni kubadilisha meneja wao, na meneja [Ange Postecoglou] waliyemleta amekuwa jibu sahihi.

"Hicho ndicho kinachopaswa kutokea Manchester United. Wanahitaji kubadilisha mtu [Ten Hag] ambaye hapati matokeo mazuri uwanjani.
 

Sherwood pia ameshangazwa ni kwanini Man U hawakufanya jitihada za kutosha kumsajili Harry Kane na Declan Rice!  kwani wangeboresha kikosi na kumfanya mwalimu aonekane bora pia.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet