Timu 9 za Afrika zafuzu hatua ya 32 Kombe la dunia
Sisti Herman
June 28, 2026
Share :

Hizi ni nchi 9 za Afrika zilizofuzu hatua ya mtoano ya 32 bora ya kombe la dunia 2026 kati jumla ya timu 10 zilizoshiriki michuano hiyo.
Ni Tunisia pekee ndiyo imeishia hatua ya makundi ya Michuano hiyo huku Afrika ikiwa bara la pili kwa timu zake nyingi kufuzu hatua ya mtoano.
- Afrika (CAF) zilishiriki timu 10, zimefuzu 9
- Ulaya (UEFA) zilishiriki timu 16, zimefuzu 13
- America kusini (COMNEBOL) zimeshiriki timu 6, zimefuzu 5
- America kaskazini (CONCACAF) zimeshiriki timu 6, zimefuzu 3
- Asia (AFC) zimeshiriki timu 9, zimefuzu 3
- Ukanda wa bahari (OFC) imeshiriki timu 1, haijafuzu





