Timu kubwa za Ulaya zamuwinda Mafoeng'
Sisti Herman
October 4, 2026
Share :

Kinda wa kimataifa wa Afrika Kusini, Relebohile Mofokeng, amezitibua akili za vigogo wa soka barani Ulaya kufuatia kiwango chake safi uwanjani.
Mwandishi wa habari za usajili, Ekrem Konur, ameripoti kuwa klabu za Atletico Madrid, Napoli, Chelsea, na Brighton & Hove Albion zinamfuatilia kwa karibu mshambuliaji huyo anayekipiga kwa sasa nchini Ubelgiji.
Mofokeng, mwenye umri wa miaka 21 na ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Royale Union Saint-Gilloise, amekuwa lulu sokoni kutokana na kasi na uwezo wake mkubwa wa kutengeneza mabao.
Wachambuzi wa soka wanaona kuwa dili la mchezaji huyo kuelekea moja ya ligi kuu tano za Ulaya liko karibu kutokana na vita hiyo ya vigogo.





