"Timu ya Taifa ni mali ya Nchi si mali ya mtu"-Makonda.
Joyce Shedrack
September 24, 2026
Share :
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema maandalizi na shughuli zinazohusu Timu ya Taifa zinahitaji uratibu wa pamoja wa taasisi zote zinazohusika ili kufikia malengo yaliyowekwa.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Makonda amesema si sahihi kwa kila taasisi au idara kuendesha mawasiliano na mikakati yake bila kushirikiana na wengine, kwa kuwa hali hiyo inaweza kusababisha mkanganyiko.
“Timu ya taifa ni mali ya nchi, sio mali ya mtu! Na sisi kama serikali tumeikasimisha kwa TFF lakini tunaendelea kuihudumia kwa posho, mishahara nk”
“Ndio maana ikitoka inapewa bendera na tunawaambia nendeni mkapambane kuipigania heshima ya nchi”.





