Timu ya U.S.A inavyotisha na Curry, James na Durant kwenye Olympic 2024
Sisti Herman
July 29, 2024
Share :
Timu ya Taifa ya Marekani ya mpira wa kikapu imeanza vyema michuano ya Olympics 2024 baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Serbia vikapu 110 kwa 84 na kufanikiwa kuongoza kundi C.
Timu hiyo iliyosheheni wachezaji bora wa ligi kuu ya mchezo huo nchini Marekani (NBA) kama;
- LeBron James aliyefunga pointi 21,Rebound 7 na Asisti 9
- Stephen Curry aliyefunga alama 11, Rebound 3 na Asisti 3
- Kevin Durant aliyefunga alama 23, Rebound 2
Wawakilishi wa Afrika Sudan Kusini wanafuatia kwenye msimamo wa kundi hilo baada ya juzi kuwatandika Puerto Rico vikapu 90-79 huku Serbia na Puerto Rico wakiwa mkiani mwa kundi.