Timu za arabuni zamtaka Bruno, yeye anafurahia kubaki Man United
Eric Buyanza
June 15, 2024
Share :
Man United watafanya mazungumzo juu ya mkataba mpya wa Bruno Fernandes atakaporejea kutoka kwenye michuano ya Ulaya.
Akiongea hivi karibuni kwenye podcast ya Football Insider, Pete O'Rourke (Mwandishi mwandamizi) alifichua kuwa timu kadhaa za Saudia zimekuwa zkitaka huduma ya Bruno, lakini mchezaji huyo bado anafurahia kusalia Man United.
Vyanzo vinasema mshambuliaji huyo anatamani kuona maboresho yakifanyika Man United ili timu ifikie malengo yake, na yeye anataka kuwa sehemu ya mipango hiyo ya mafanikio.