Timu za Saudi Arabia zaandaa ofa mpya kwa Mo Salah.
Joyce Shedrack
December 6, 2025
Share :
Mohamed Salah ameripotiwa kuwindwa na vilabu kadhaa vya Saudi Arabia kabla ya dirisha la usajili la Januari mwaka ujao.
Mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Misri, hajaanza mechi mbili zilizopita za ligi na ripoti zinasema kuwa anaweza kushawishika kuondoka Anfield.
Taarifa kutoka Saudia zinaripoti kuwa vilabu kadhaa vya Nchini humo viko tayari kuwasilisha ofa mpya kwa ajili ya Salah, kufuatia nia ya awali kwa nyota huyo wa Liverpool. Hata hivyo, inasemekana kwamba ingawa fedha zinaweza kupatikana, ofa yoyote haitakuwa karibu na ofa ya Al-Ittihad ya pauni milioni 200, ambayo ilikataliwa mwaka 2023.
Kiwango cha Mo, kutokuwa na furaha kwa kutokuwa kwenye timu, hitaji la Liverpool kubadilisha kitu na ukweli kwamba wana washambuliaji wengi, yote yanasaidia kumsukuma kwenda Mashariki ya Kati.





