pmbet

Timu zinavyotega mitego wakizuia (Pressing Traps & Trigger)

Sisti Herman

July 22, 2024
Share :

Kwenye mbinu za uchezaji wa Mpira wa miguu kuna namna tofauti za uzuiaji, kuzuia kwa shinikizo la kubwa au la juu (High Pressure Difensive Style or Pressing) na kuzuia kwa shinikizo dogo au la chini (Low pressure Difensive Style) ambayo mara nyingi uzuiaji wake huanzia kwenye theluthi ya pili ya uwanja kwa timu inayozuia

 

Leo tutajadili uzuiaji wa shinikizo kubwa au la juu (Pressing) ambayo ni namna ya uzuiaji ambapo timu inayozuia hushinikiza kwa lazima wachezaji wa timu inayoshambulia kupoteza umiliki wa mpira kwa kumyima muda na nafasi ya kuendelea kumiliki mpira

 

Ili "Pressing" iweze kufanywa kwa usahihi kuna viambata vikuu viwili ambavyo huweza kuwa sababu kuu ya timu inayoshambulia kupoteza umiliki wa mpira, navyo ni Kichochezo cha shinikizo (Pressing Trigger) na Mtego wa shinikizo (Pressing Trap) 

 

Kichochezo cha shinikizo (PRESSING TRIGGER)

 

Ili timu inayozuia iweze kushinikiza timu inayoshambulia kupoteza umiliki wa mpira ni lazima wachezaji na waalimu wa timu inayozuia waweze kujua baadhi ya madhaifu ya timu inayoshambulia ili viweze kuwa chanzo cha wao kuanzisha kuwashinikiza kupora mipira

 

Vichocheo ni pamoja na kujua wachezaji wasio na uwezo mzuri kumiliki mpira wakati wakiwa wameshikizwa (under pressure), mchezaji kuumiliki mpira upande ambao sio wa mguu bora anaoutumia mara kwa mara, pia wachezaji kupiga pasi za nyuma

 

Mtego wa shinikizo (PRESSING TRAP)

 

Baada ya timu pinzani kujua kichocheo cha kuweza kuanzisha shinikizo (Pressing Trigger), wanaweza sasa kutumia madhaifu hayo kimbinu kwa kuweza kutega mitego ili kuweza kutumia vichocheo kurudisha mpira kwenye umiliki wao

 

Namna tofauti za kutega mitego kulingana na vichocheo ni pamoja na kulazimisha mchezaji wa timu inayoshambulia asiyekua na uwezo wa kumiliki mpira wakati wakiwa wameshikizwa kupewa mpira kwa wao kuwazuia wachezaji wote wenye uwezo huo na kumuacha huyo asiyekua na uwezo mkubwa ili akipewa mpira wamshambulie kwa kasi na idadi kubwa

 

Pia kulazimisha mchezaji kutumia upande wa mguu ambao hautumii mara kwa mara kushambulia, pia kulazimisha timu inayoshambulia kurudisha mpira nyuma 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet