Timu zingine mwiko kuvaa soksi nyeupe Darajani
Sisti Herman
March 15, 2026
Share :

Wiki hii, Machi 10,2026 Chelsea FC waliadhimisha kutimiza miaka 121 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo, iliyozaliwa tarehe 10 Machi 1905 katika pub moja jijini London iliyojulikana kama The Rising Sun, ambayo kwa sasa inaitwa The Butcherโs Hook.
Katika historia ya klabu hiyo pia kuna utamaduni wa kipekee unaohusiana na sare zao wanapocheza nyumbani katika dimba la Stamford Bridge.
Soksi nyeupe zimekuwa sehemu ya utambulisho wa Chelsea tangu katikati ya miaka ya 1960, wakati aliyekuwa kocha wa timu hiyo Tommy Docherty alipobadilisha muonekano wa kikosi kwa kuunganisha jezi ya bluu, kaptura ya bluu na soksi nyeupe. Muonekano huo uliibuka kuwa alama maarufu ya klabu hiyo.
Kutokana na utambulisho huo, timu zinazotembelea Stamford Bridge haziruhusiwi kuvaa soksi nyeupe wanapocheza dhidi ya Chelsea nyumbani. ๐๐ง๐๐๐ฉ๐จ ๐ฌ๐๐ซ๐ ๐ฒ๐๐จ ๐ข๐ง๐ ๐ฌ๐จ๐ค๐ฌ๐ข ๐ก๐ข๐ณ๐จ, ๐ก๐ฎ๐ฅ๐๐ณ๐ข๐ฆ๐ข๐ค๐ ๐ค๐ฎ๐๐๐๐ข๐ฅ๐ข๐ฌ๐ก๐ ๐ค๐๐๐ฅ๐ ๐ฒ๐ ๐ค๐ฎ๐๐ง๐ณ๐ ๐ค๐ฐ๐ ๐ฆ๐๐ก๐๐ณ๐จ.
Ingawa inaweza kuonekana kama sheria ya ajabu, sababu yake ni ya kiufundi zaidi, kwani kanuni za matangazo ya televisheni zinahitaji timu mbili uwanjani zitofautishwe kwa urahisi ili watazamaji waweze kuzitambua bila shida wakati wa mchezo.





