Tin White azichapa na mdeni wake kweupee
Eric Buyanza
February 17, 2024
Share :
Nguli kunako tasnia ya komedi hapa Bongo, Tin White, amezichapa ngumi kweupe kabisa na msanii Bongo flava aliyefahamika kwa jila la YJ kisa kikielezwa kuwa ni mtonyo (pesa) ambazo Tin white amekuwa akimdai YJ kwa muda mrefu na kuzungushwa kila kukicha.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, YJ, alimfanyisha kazi Tin White ya kutokea kama (Video King) kwenye video ya mwanamuziki huyo lakini hakupewa malipo kama walivyokubaliana na ndipo Tin white alipochoshwa na hali hiyo ya kuzungushwa na kuamua kutimba nyumbani kwa YJ kudai haki yake hali iliyosababishwa vurugu kati yao.
YJ naye amemshtumu Tin White kwa kuvamia nyumbani kwake na kufanya fujo ikiwa ni pamoja na kuvunja TV na simu.