pmbet

TMA yatoa tahadhari mvua za Vuli na El Nino

Sisti Herman

August 18, 2026
Share :

 

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imezitaka Mamlaka zinazosimamia miundombinu ya usafiri, ikiwemo reli, barabara, bandari na usafiri wa anga kujiandaa kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za Vuli zinazotarajiwa katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2026.

TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, Ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma, huku msimu huo ukitarajiwa kuathiriwa kwa kiwango kikubwa na hali ya El Niño yenye nguvu.

Akitoa utabiri huo leo Agosti 18, 2026, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a amesema vipimo vya joto la bahari katika eneo la Niño 3.4 vilifikia nyuzi joto 2.2 mwezi Agosti na vinatarajiwa kuongezeka hadi nyuzi joto 3.6 ifikapo Desemba 2026.

Kwa upande wa usafiri, Chang’a amesema reli ya mwendokasi (SGR), reli ya kawaida (MGR), barabara na madaraja pamoja na shughuli za bandari ni miongoni mwa maeneo yanayoweza kuathiriwa kutokana na mafuriko na mmomonyoko wa udongo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet