Tom Holland apata ajali akiigiza kama Spider Man.
Joyce Shedrack
September 23, 2025
Share :
Tom Holland alilazwa hospitalini kwa muda mfupi baada ya kupata mtikiso wa ubongo wakati akiwa kwenye seti ya filamu Spider-Man Brand New Day.
Ajali hiyo ilitokea Ijumaa iliyopita asubuhi katika Leavesden Studios huko Watford, huku gari la wagonjwa likifanikiwa kumkimbiza mwigizaji huyo hospitalini.
Hata hivyo utayarishaji wa filamu hiyo ulisitishwa lakini wadadisi wanasema kulazwa hospitalini siyo kwamba amepatwa na tatizo kubwa sana ni kama tahadhari tu na hivyo anatarajiwa kurejea kazini ndani ya siku chache.
Filamu mpya ya Spider-Man, inatarajiwa kuachiliwa mnamo Julai 24, 2026.





