pmbet

Toni Kroos ausha jiwe gizani Real Madrid kisa Sub ya Dembele.

Joyce Shedrack

May 9, 2026
Share :

Nyota wa zamani wa Real Madrid na Ujerumani Toni Kroos ametoa maoni yake kuhusu mchezo wa Bayern Munich na PSG uliopigwa Ujerumani huku akiguswa na nyota Ousmane Dembele ambaye licha ya kufanyiwa mabadiliko dakika ya 65 na kocha wake  hakuonesha kukasirishwa na jambo hilo.

Toni Kroos appears to aim subtle dig at Kylian Mbappe & Vinicius Junior  over lack of defensive work at Real Madrid | Goal.com

Kroos amesema Dembele ambaye ni mchezaji bora wa Dunia alitolewa nje na kuendelea kushirikiana na wenzake kwa furaha huku akilinganisha na wachezaji wengine ambao wamekuwa wakikasirika wakifanyiwa mabadiliko na baadhi ya mashabiki wakitoa maoni yao kwamba Nguli huyo amewalenga baadhi ya nyota wa Real Madrid.

 

“Luis Enrique amemtoa Ousmane Dembélé, ambaye ni mchezaji wake bora, dakika ya 65 ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na hakuna mtu aliyelalamika" 

 

“Anatoka uwanjani, anapeana mkono na kocha wake, kisha anakaa benchi akiwashangilia wachezaji wenzake kana kwamba yeye ni mmoja wa benchi la ufundi. Kuna baadhi ya mifano ya kinyume na hili” 

 

“Unamtazama Ousmane Dembélé jinsi anavyowapigia kelele wachezaji wenzake waendelee kupambana akiwa benchi. Hivyo siyo ambavyo 90% ya wachezaji wanaojiona mastaa hufanya. Wao huanza kuonyesha ishara mbaya uwanjani, halafu wakikaa benchi wanakuwa wamekasirika na kununa.”

 

Unadhani ujumbe wa Kroos ni kwa ajili ya wachezaji gani wa Real Madrid?.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet