Tony Rashid apigwa TKO Ubelgiji
Sisti Herman
February 4, 2024
Share :
Bingwa wa zamani wa ABU, Tony Rashid amepoteza pambano la kuwania mkanda wa ubingwa wa IBO Intercontinental kwa kichapo cha TKO ya raundi ya nane katika pambano la raundi kumi dhidi ya Hovhannes Martirosyan wa Ubelgiji.
Tony amepoteza pambano hilo lililopigwa kwenye Ukumbi wa Hasselt uliopo Limberg, Ubelgiji ambalo limeisha muda mfupi ulioisha.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mtanzania huyo kupoteza pambano nje ya mipaka ya Tanzania akiwa katika bara la Ulaya.