Tony Rashid kuupigania Ubingwa wa ABU Afrika kusini
Sisti Herman
June 4, 2025
Share :
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Tony Rashid anatarajiwa kupanda ulingoni katika pambano lake litakalofanyika nchini Afrika Kusini.
Rashid atapigana dhidi ya bondia Asanda Ginqi katika pambano la raundi 10 kwaajili ya kuwania ubingwa wa ABU katika uzani wa ‘light weight’.
Rashidi kutoka Tanzania anatarajiwa kushiriki katika pambano hilo la Juni 20 mwaka huu ambalo litafanyika Afrika Kusini katika jiji la East London ambapo ndipo kitovu cha mchezo wa ngumi nchini humo.
Rashid amecheza mapambano 23 akishinda 17 na 11 kwa ‘KO’, akipoteza mara tatu na mawili kwa ‘KO’ na akitoka sare mara tatu.
Pia Rashid ni bondia namba mbili nchini Tanzania kati ya mabondia 95 katika uzani wa ‘Super feather’ huku Duniani akiwa namba 138 kati ya 1991 akiwa na hadhi ya nyota mbili na nusu.
Kwa upande wa mpinzani wake Ginqi ni bondia namba mbili kwao Afrika Kusini kati ya mabondia 33 na Duniani ni wa 91 kati ya mabondia 1991 akiwa na hadhi ya nyota mbili na nusu akiwa amecheza mapambano 15 akishinda 14 huku 9 akishinda kwa KO na kupoteza pambano moja.
Pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa Border conference huku kiingilio kwa VIP kikiwa ni Rand 500 ambayo ni sawa na 75,000 kwa pesa ya Tanzania na tiketi za kawaida ni Rand 200 ambayo ni sawa na 30,000.