TPLB, TFF yawapokea ndugu zake Doumbia wa Simba kutoka Mali
Eric Buyanza
August 25, 2026
Share :

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wamewapokea Abidane Issa Sangare na Niama Loua Berete kutoka nchini Mali anapotokea mshambuliaji nyota wa Simba, Ibrahim Doumbia.
Wageni hao Abidane Issa Sangare na Niama Loua Berete ni ugeni wa wawakilishi wa Chama cha Mpira wa Miguu kutoka nchini humo waliokuja nchini kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi (TPLB).
TPLB na TFF zimekuwa zikipokea wawakilishi mbalimbali wa mashirikisho kwa ajili ya kuongeza ujuzi wa jinsi wa kuendesha mambo ya mpira.





