TRA kutumia mbio za Mwenge kutoa elimu ya kodi
Eric Buyanza
April 2, 2024
Share :
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imejipanga kutoa elimu ya kodi, kusikilza changamoto na kujibu maswali katika maeneo yote ambayo mwenge utalala.
Afisa mkuu wa usimamizi wa kodi kutoka makao makuu TRA, Hamady Mteri ameyasema leo Aprili 2, 2024 wakati wa uzinduzi wa mbio za mwenge uliofanyika katika viwanja vya Ushirika vilivyopo Moshi mkoani kilimanjaro.
Mteri amesema Mwenge unauhusiano mkubwa na kodi kwani ukimbizaji wa mbio za mwenge unaenda sambamba na uwekaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ambapo utekelezaji wake utahitaji fedha ambapo kodi ndio chanzo kikuu cha pato la taifa.
Awali, Katibu wa waendesha bodaboda mkoani hapo Rashid Omary ameishukuru TRA kwa kushiriki katika mbio za mwenge na kuwaomba wananchi kufika katika banda la TRA kwa lengo kujifunza mambo mbali mbali ya kodi.
Nae modistus Malya amesema kodi ni maendeleo hivyo amewataka wananchi wanaofanya biashara kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa.