TRA yakusanya Tril. 9.31 Robo ya mwisho wa mwaka wa fedha 2025/26
Sisti Herman
April 2, 2026
Share :

Tanzania Revenue Authority (TRA) imekusanya Sh9.31 trilioni kati ya Januari na Machi 2026, kiwango kilichozidi lengo la Sh8.75 trilioni katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/26.
Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuf Mwenda, amesema makusanyo hayo yanaonyesha ufanisi wa mifumo ya ukusanyaji kodi, kuongezeka kwa utii wa walipa kodi na mageuzi ya taasisi yanayolenga kupanua wigo wa kodi.
Kwa mujibu wa TRA, mafanikio hayo yanaashiria ufanisi wa asilimia 106.4 katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, huku mwezi Machi pekee ukikusanya Sh3.58 trilioni dhidi ya lengo la Sh3.32 trilioni.





