Traore akanusha kuwepo kwa mgawanyiko kwenye Jeshini
Eric Buyanza
June 22, 2024
Share :
Kiongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso, Ibrahim Traore amekunusha madai ya kuwepo kwa mgawanyiko ndani ya jeshi la nchi hiyo, siku chache baada ya milio ya risasi kuskika karibu na makaazi yake na kombora kurushwa karibu na kituo cha habari cha kitaifa.
Traore ametoa kauli hii baada ya kutembelea runinga ya kitaifa ya RTB kulikorushwa kumbora juma moja lililopita, akisema kombora hilo lilirushwa kimakosa na walinzi wa kituo hicho.
Matukio haya yanakuja siku chache tangu wanajeshi wa nchi hiyo zaidi ya 100 kuuawa na wana-Jihadi karibu na mpaka wa Niger.