Traore apiga marufuku ushoga Burkina Faso
Sisti Herman
September 2, 2025
Share :
Nchini Burkina Faso, utawala wa kijeshi kwa kauli moja umepitisha sheria inayoharamisha vitendo vya ushiga kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi.
Sheria hiyo inatoa kifungo cha karibu miaka mitano jela kwa watu watakaopatikana wakijihusisha na ushoga.
Takriban nchi 30 za Afrika zimeharamisha vitendo hivyo, suala ambalo halikuwa limepigwa marufuku nchini Burkina Faso kabla ya Captaine Ibrahim Traore kuchukua madaraka miaka mitatu iliopita.