Traore awaambia wananchi, msahau kuhusu demokrasia
Eric Buyanza
April 4, 2026
Share :

Kiongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore amewaambia wananchi wa taifa hilo la Afrika Magharibi kwamba lazima wasahau kuhusu demokrasia. Traore amesema hayo katika mahojiano yaliyotangazwa kwenye televisheni ya kitaifa nchini humo ya RTB.
Akitolea ufafanuzi kauli yake, Traore amesema kwamba watu wa Burkina Faso wanahitaji kusahau suala hilo sababu msingi wa demokrasia yenyewe sio kwa ajili yao.
Itakumbukwa kwamba kiongozi huyo alichukua madaraka kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi mnamo Septemba 2022 baada ya kuiangusha serikali nyingine ya kijeshi, na tangu wakati huo amezuia sauti za wapinzani.
Serikali ya kijeshi ilivunja tume ya uchaguzi ya nchi hiyo mwaka jana na kisha mwezi Februari. Bunge lililoongozwa na wanajeshi pia lilipiga marufuku vyama vyote vya siasa, ambavyo shughuli zake zilikuwa zimesimamishwa tangu 2022. Hata hivyo, Umoja wa Mataifa umeitaka Burkina kubatilisha uamuzi wa kupiga marufuku vyama vya siasa na kukomesha ukandamizaji.





