Travis Scott aitangaza album yake kupitia michuano ya Kombe la Dunia.
Joyce Shedrack
June 25, 2026
Share :
Wakati Mashabiki wengi wa soka wakizungumzia kuhusiana na matukio mengi ya kimichezo yanayoendelea kwenye Kombe la Dunia ikiwemo Performance ya Cristiano Ronaldo kwenye mchezo wa Ureno dhidi ya Uzbekistan Rapa @travisscott alifanikiwa kuiba sehemu ya mjadala huo baada ya kupiga picha akiwa na watoto wake Stormi na Aire.

Picha hio ndiyo iliyoibua mijadala kutokana na kuonekana na iPod yenye Album yake mpya, na hii ni baada ya kuzungumza na Mtangazaji kwenye Finali za Champion Ligi alipoulizwa kuhusiana na kubeba iPod kwa namna kama hiyo akisema kuwa ameweka Album yake kwenye iPod ili iwe salama zaidi.
Kutokana na uhudhuriaji wake kwenye majukwaa makubwa ya Kimichezo Travis amechukulia kama fursa katika kujipatia mashabiki wapya na hata kuendelea kuukuza Muziki wake na kujulikana zaidi na kufanya watu wawe na attention naye kuelekea kuachia Album yake kwahiyo ni sehemu ya ku-promote biashara yake.





