TRC Yatangaza kurejea kwa huduma ya SGR.
Joyce Shedrack
October 23, 2025
Share :
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza rasmi kurejea kwa huduma za usafiri wa treni za SGR zilizokuwa zimesimama asubuhi ya leo kutokana na ajali iliyotokea kituo cha Ruvu kutokana na hitilafu ya kiuendeshaji.
Shirika linaomba radhi wateja wake kwa usumbufu uliojitokeza na pia linawashukuru kwa uvumilivu wao.
Huduma bora kwa wateja wetu ndiyo kipaumbele cha Shirika.





