Treni ya umeme Dar-Dodoma kuanza rasmi mwezi julai
Eric Buyanza
February 27, 2024
Share :
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema treni za umeme zitaanza kutoa huduma ya usafiri kuanzia mwezi Julai, mwaka huu.
Ikumbukwe kuwa Desemba 31, mwaka jana, Rais Samia Suluhu Hassan aliielekeza Wizara ya Uchukuzi kuhakikisha kuwa ifikapo mwisho mwa Julai, mwaka huu treni za umeme zianze kutoa huduma kwa wasafiri kati ya Dar es Salaam na Dodoma.