Trent na Carvajal kuwa fiti kukiwasha dhidi ya Barcelona.
Joyce Shedrack
October 16, 2025
Share :
Walinzi wa Kulia wa klabu ya Real Madrid Dani Carvajal na Trent Alexander Arnold wameanza mazoezi ya kurejea uwanjani baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yanawakabili.
Nyota hao wanaendelea kufanya mazoezi huku wakiwa chini ya uangalizi wa madaktari wa klabu hiyo ili wawe fiti mapema kurejea uwanjani kwa ajili ya michezo ya ligi.
Real Madrid wataikabili Fc Barcelona kwenye mchezo wa ligi kuu Nchini humo Oktoba 26 katika uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu.