pmbet

Trump aanza vyema safari ya kurudi Ikulu

Eric Buyanza

January 17, 2024
Share :

Donald Trump ameanza vyema safari yake ya kurejea Ikulu ya Marekani, baada ya kushinda uchaguzi wa kwaza wa mchujo katika jimbo la Iowa kuwania uteuzi wa chama cha Republican kugombea urais mwezi Novemba mwaka huu huku mpinzani wake gavana wa Florida DeSantis safari yake ikiwa mashakani baada ya kufanya vibaya kwenye kura ya kwanza ya mchujo huo.

Licha ya kuwekeza sana muda na rasilimali kwenye jimbo hilo, la kwanza kuanza uchaguzi wa mchujo wa vyama nchini Marekani, DeSantis alimaliza akiwa ameachwa nyuma kwa takribani asilimia 30 na Donald Trump, na akiwa amempita kidogo sana anayemufuatia, balozi wa zamani wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Nikki Haley. DeSantis, alipata asilimia 21, Haley akiwa na asilimia 19, lakini Trump aliwapiku akiwa na asilimia 51.

Kirk Jowers, ambaye amekuwa kwenye kampeni za marais watano wa Republican na ambaye ni mshauri wa wafadhili wa DeSantis, anaona kwamba kwa mgombea wake huyo mambo yamekwisha.

Kirk anasema "Matokeo ya Iowa yanathibitisha bila tone la shaka kwamba Trump ndiye atakayekuwa mgombea na hakuna yeyote awezaye kuzuia hilo, isipokuwa Mungu au mahakama." 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet