pmbet

Trump aikubalia Pakistan, aagiza jeshi lake kutoishmbulia Iran

Eric Buyanza

April 22, 2026
Share :

Rais wa Marekani, Donald Trump, hapo jana alitangaza kuongeza muda wa usitishaji mapigano na Iran ili kutoa nafasi ya majadiliano, wakati huu makubaliano ya awali yakimalizika bila ya tukio lolote la makabiliano.

 

Uamuzi wa Trump kutoa nyongeza hii ambayo sasa itakuwa kwa muda usiojulikana, amesema ulitokana na maombi ya Pakistan ambayo ni mpatanishi mkuu katika mgogoro wake na Iran, akisisitiza haja ya kuipta Tehran muda zaidi kuwasilisha mapendekezo yenye tija kumaliza vita.
 

Awali rais Trump alikuwa amesema hatoongeza hata chembe ya muda kwa Iran ikiwa mpaka kufikia leo itakuwa haijakubali mkataba wa usitishaji mapigano, hii ikiwa ni mara ya pili kwa kiongozi huyo kubadili msimamo wake kuhusu Iran.
 

Katika andiko alilochapisha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, rais Trump amesema ameliagiza jeshi kutoishambulia Iran baada ya muda wa awali wa usitishwaji mapigano kumalizika, lakini akalitaka kuendelea kutekeleza zuio la meli kuingia na kutoka kwenye bandari ya Iran.
 

Tangazo la Marekani limekuja saa chache tangu utawala wa Tehran usema hautahudhuria mazungumzo ya Islamada yaliyokuwa yafanyike jana na Leo, kwa kile umedai muendelezo wa Washington kukiuka Ahadi zake.

 

Wachambuzi wa mambo wanasema uamuzi wa Marekani unaweza kutafsirika pengine kama mbinu ya Trump kujipa muda kujipanga tena kabla ya kufanya mashambulio ya kushtukiza dhidi ya Iran.


 

RFI

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet