pmbet

Trump amfagilia Musk kwa kupunguza gharama za serikali

Eric Buyanza

February 4, 2025
Share :

Rais wa Marekani, Donald Trump amempongeza Bilionea Elon Musk, ambaye anaongoza Idara mpya ya Ufanisi wa Serikali (DOGE) kwa juhudi zake za kupunguza bajeti ya serikali.

Katika mahojiano na Fox News yaliyoruka siku ya Jumapili, Februari 2, Trump alisifu juhudi za Musk katika kupunguza gharama za ziada za serikali.

“Nadhani Elon anafanya kazi nzuri. Yeye ni mkataji mkubwa wa gharama. Wakati mwingine hatukubaliani naye, kwa kutokwenda anakotaka kwenda, lakini anafanya kazi nzuri… ni mtu mwerevu… anajaribu sana kupunguza bajeti ya serikali yetu.” alisema Trump

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet