pmbet

Trump anabadilisha biashara kuwa mchezo wa kulipa kisasi - China

Eric Buyanza

April 3, 2025
Share :

Baada ya kutangaza ushuru mkubwa kwa mataifa mbalimbali duniani ikiwemo China, Wizara ya Biashara ya nchi hiyo imeitaka Marekani "kufuta mara moja hatua hizi za ushuru wa upande mmoja na kutatua mizozo ya kibiashara ipasavyo kwa njia ya mazungumzo sawa na washirika wake". 

"China inapinga vikali hatua hii na itachukua hatua madhubuti ili kulinda haki na maslahi yake," msemaji alisema. 

Hapo awali, Shirika la Habari la China Xinhua lilichapisha maelezo likiita ushuru huo "unyanyasaji wa kujishinda" na kusema Trump "anabadilisha biashara kuwa mchezo wa kulipa kisasi. 

Huenda China ndiyo nchi ambayo imeathirika zaidi baada ya tangazo la Trump leo, ikiwa na ushuru wa ziada wa 34% kwa bidhaa zote za China zinaouzwa Marekani.

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet