Trump anaweza kushtakiwa, hana kinga ya Urais
Eric Buyanza
February 7, 2024
Share :
Aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump hana kinga ya urais na anaweza kufunguliwa mashtaka ya kupanga njama ya kutengua matokeo ya uchaguzi wa 2020, mahakama ya Marekani imeamua.
Bw Trump alikuwa amedai katika kesi hiyo kwamba hawezi kushtakiwa kwa makosa ya jinai kwa vitendo alivyosema viko chini ya majukumu yake kama rais.
Lakini uamuzi wa Jumanne huko Washington DC ulifuta madai hayo.
Ni kikwazo kwa Bw Trump ambaye kwa miaka mingi ametaja kinga ya rais huku akikabiliana na kesi nyingi.
Rais huyo wa zamani anatarajiwa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo, ikimaanisha kwamba kesi hiyo inaweza hatimaye kwenda katika Mahakama ya Juu ambapo wahafidhina wanapata wingi wa 6-3.
Wakili Maalum wa Marekani Jack Smith amemshtaki Bw Trump kwa kula njama ya kubatilisha ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa 2020 na kufanya udanganyifu ili kubakia madarakani.