pmbet

Trump anusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi

Sisti Herman

July 14, 2024
Share :

Aliyekuwa Rais wa Marekani awamu iliyopita na mgombea Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao wa nchi hiyo Donald Trump amejeruhiwa kwa kupigwa risasi wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mjini Butler, Pennsylvania.

 



Donald Trump ambaye ni mgombea urais mtarajiwa kupitia chama cha Republican, alionekana akinyoosha mkono wa kulia kuelekea shingoni mwake kabla ya shambulizi hilo kutokea huku mfululizo wa milio ya risasi ikisikika

Maafisa wa ulinzi wa rais kwa haraka walikimbilia kwenye jukwaa kujaribu na kumzingira kiongozi huyo huku hali ya wasiwasi ikionekana kutanda.

Damu ilionekana usoni mwake na kwenye sikio lake la upande wa kulia ambapo alikimbizwa nje ya jukwaa haraka na maafisa wa kitengo cha Secret Service.

Katika chapisho lake kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump alisema risasi ilipenya “sehemu ya juu” ya sikio lake la kulia. Hapo awali, msemaji wake alisema “anaendelea vizuri” na anapokea matibabu katika kituo cha matibabu cha eneo hilo

Watu wawili wameuwawa katika tukio hilo akiwemo mdunguaji aliyempiga risasi Donald Trump ambaye aliyepigwa risasi na kufa katika eneo la tukio na maafisa wa usalama.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet