pmbet

Trump apita na upepo, aingiza sokoni raba ya tukio lale la kupigwa risasi

Eric Buyanza

July 18, 2024
Share :


Kuwa mfanyabiashara mkubwa duniani sio jambo rahisi...kwasababu inakubidi uwe na jicho na ujanja pia wa kuchungulia na kutambua fursa kila kona, hilo amelithibitisha tajiri mkubwa na mgombea Urais wa marekani Donald Trump. 

Ni hiviii....siku chache baada ya Rais huyo wa zamani wa marekani kunusurika katika jaribio la mauaji akiwa kwenye mkutano wa kampeni huko Butler, Pennsylvania, kampuni anayoimiliki imeingiza sokoni raba zenye picha ya tukio hilo ikimuonyesha Trump akiwa na damu inayochuruzika kwenye shavu huku akiwa ameinua ngumi juu baada ya kupigwa risasi sikioni.

Raba hizo zinauzwa Dollar $299 (sawa na shilingi 793,510/=) na zimetengenezwa pea 5,000 pekee.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet