Trump asema anaweza kukiteka kisiwa cha kharg cha Iran
Eric Buyanza
March 30, 2026
Share :

Rais wa Marekani Donald Trump ameliambia gazeti la Financial Times kwamba anaweza "kuchukua mafuta nchini Iran" na ikiwezekana akakiteka Kisiwa cha Kharg ambacho ni kitovu kikuu cha mafuta nchini humo.
"Kusema ukweli, jambo ninalotaka zaidi ni kuchukua mafuta nchini Iran lakini baadhi ya watu wajinga huko Marekani wanasema: 'Kwa nini unafanya hivyo?' Lakini ni watu wajinga," alisema.
Trump alipendekeza hatua hiyo inaweza kumaanisha kuchukua kisiwa cha Kharg. "Pengine tuchukue Kisiwa cha Kharg, au tuachane nacho. Tuna chaguzi nyingi," Trump aliambia Financial Times. “Inamaanisha pia kuwa tulipaswa kuwa huko [katika Kisiwa cha Kharg] kwa muda.”
Alipoulizwa kuhusu ulinzi wa Iran katika kisiwa hicho alisema: "Sidhani kama wana utetezi wowote. Tunaweza kukichukua kwa urahisi sana."
Kauli hiyo ya rais inakuja huku wanajeshi 3,500 zaidi wa Marekani wakiwasili Mashariki ya Kati, hofu ya wanajeshi wa Marekani kijiunga na mashambulizi ya Iran ikiongezeka.
Trump aliongeza kuwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Marekani na Iran kupitia "mabalozi" wa Pakistan yalikuwa yanaendelea vizuri, lakini hakugusia suala makubaliano ya kusitisha mapigano yanaweza kufikiwa hivi karibuni.
"Mkataba unaweza kufikiwa haraka," alisema.
BBC





