pmbet

Trump asema hataki kushughilika tena na Iran, ni wagonjwa

Eric Buyanza

July 8, 2026
Share :

Jeshi la Marekani limesema limefanya mashambulizi mapya dhidi ya Iran mapema Jumatano, saa chache baada ya meli tatu za kibiashara kushambuliwa katika Mlango Bahari wa Hormuz.

 

Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X na Kamandi Kuu ya jeshi la Marekani, CENTCOM imesema vikosi vya Marekani vilianzisha mashambulizi hayo kwa kuyalenga zaidi ya maeneo 80.

 

Kulingana na CENTCOM, mashambulizi hayo yaliilenga mifumo ya ulinzi wa anga ya Iran, mifumo ya ufuatiliaji wa pwani, makombora ya kutokea ardhini hadi angani, makombora ya kushambulia meli na maeneo ya kurushia droni, na zaidi ya boti ndogo 60 za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, IRGC.


Kwa upande wa Rais Trump amesema leo Jumatano kuwa Hati ya Makubaliano iliyosainiwa kati ya Marekani na Iran ili kuumaliza mzozo huo imekwisha.

"Kwangu mimi, nadhani yameisha. Ni kupoteza muda. Sitaki kushughulika nao tena. Ni wagonjwa. Wanaongozwa na wagonjwa, na ni watu wagomvi na katili" alisisitiza Trump.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet