pmbet

Trump asema hataki wasomali Marekani

Eric Buyanza

December 3, 2025
Share :

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hataki wahamiaji wa Kisomali nchini Marekani, na kuwaambia waandishi wa habari wanapaswa "kurejea walikotoka."

"Siwataki katika nchi yetu, nitakuwa mkweli," amesema wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri siku ya Jumanne. Trump amesema Marekani "itaharibika ikiwa tutaendelea kuchukua takataka katika nchi yetu."

Maoni yake ya kudhalilisha yanakuja wakati maafisa wa uhamiaji wakiripotiwa kupanga operesheni katika jamii kubwa ya Wasomali ya Minnesota.

Maafisa katika jimbo hilo wamekosoa mpango huo, wakisema unaweza kuwaondoa isivyo haki raia wa Marekani ambao wanatoka katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Minneapolis na St Paul, ambazo kwa pamoja zinajulikana kama Twin Cities, ni nyumbani kwa mojawapo ya jumuiya kubwa zaidi za Wasomali duniani na kubwa zaidi nchini Marekani.

Maoni yake ya siku ya Jumanne, ambayo yalikuja mwishoni mwa mkutano wa baraza la mawaziri, Trump alisema: "Siwataki katika nchi yetu. Nitakuwa mkweli kwa hilo. Mtu atasema, 'Loo, hiyo si sahihi kisiasa.' Sijali siwataki katika nchi yetu."

"Nchi yao ya Somalia unajua hawana chochote. Wanakimbia huku na huko kuuana," Trump alisema.

Kisha akageukia kumkosoa Mbunge Ilhan Omar, wa chama cha Democratic, ambaye ni Mmarekani mwenye asili ya Somalia, ambaye amekuwa akigombana naye mara kwa mara.

"Siku zote huwa namtazama," Trump alisema, akiongeza kuwa Omar "anamchukia kila mtu. Na nadhani ni mtu asiye na uwezo."

"Kuniandama kwake kunatisha," Omar alisema katika chapisho katika mtandao wa kijamii. "Natumai atapata msaada anaohitaji."

Idara ya Uhamiaji ya Marekani (ICE) imeagizwa na utawala wa Trump kuwalenga wahamiaji wa Kisomali wasio na vibali katika Twin Cities, mtu anayefahamu mipango hiyo ameliambia shirika la habari la CBS News siku ya Jumanne.

Mamia ya watu wanatarajiwa kulengwa operesheni itakapoanza wiki hii, afisa huyo alisema. Gazeti la New York Times liliripoti kwa mara ya kwanza operesheni hiyo.

Kulingana na viongozi wa eneo hilo, kuna takriban watu 80,000 wanaoishi huko ambao asili yao ni kutoka Somalia, na wengi wao ni raia wa Marekani.

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet